Quality Centre—Uchumi

Uchumi wa mambo ya kale Uchumi wa mambo ya kale Uchumi wa mambo ya kale Uchumi wa mambo ya kale Uchumi wa mambo ya kale Uchumi wa mambo ya kale Uchumi wa mambo ya kale

PM Majaliwa meets Quality Group Limited management

Honorable Kassim Majaliwa, Tanzanian Prime Minister, meets Quality Group (QGL) Limited to discuss Group’s initiatives and updates

Caption for slide three slide three slide three

own descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptionsown descriptions

Caption for slide four Caption for slide

own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions

Caption for slide five Caption for slide five

own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions own descriptions

Monday, November 28, 2016

Hon. Kassim Majaliwa, Tanzanian Prime Minister, meets Quality Group (QGL) Limited to discuss Group’s initiatives and updates on the Two Sugar Plants, Investments in Manufacturing Transformers, Smart Meters and Concrete Poles with biggest global players in the Industry, e-Governance, Technology transfer for Health sector and Establishment of Health Clinics. QGL also proposed a Global Investor meet in Tanzania for Mining, Tourism and Health to bring serious Investors from all over the world. On his right Mr. Monish, Mr. Stavros Isaakidis, Mr. Maurizio Mian and Mr. Arif.

Quality Group kuunganisha matrekta nchini

 KAMPUNI ya Quality Group Limited (QGL) imeingia ubia na kampuni ya kimataifa ya India iitwayo International Tractors Limited (Sonalika) kwa ajili ya kuanza kuunganisha matrekta ya Sonalika nchini.

Akizungumza jana Dar es Salaam, kwenye hafla ya kusaini  makubaliano hayo, Ofisa Uendeshaji Mkuu wa QGL, Constantinos Vasileiadis alisema makubaliano hayo yanalenga kuinua sekta ya kilimo kwa kuunganisha matrekta nchini na kupunguza gharama za ununuzi.

“Tumesaini makubaliano na International Tractors Ltd ili kuanza kuunganisha matrekta ya Sonalika nchini, ikiwa ni juhudi za kuchochea maendeleo ya viwanda ambavyo vitasababisha kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” alisema.

“Pia, uunganishaji huo wa matrekta utapunguza gharama   ambazo wakulima walikuwa wakizipata katika ununuzi wa nyenzo hizo za kilimo.

“Zitauzwa kwa gharama nafuu zaidi, hivyo kuwa kichocheo cha wakulima kuondokana na jembe la mkono,” alisema Vasileiadis.

Aidha, Vasileiadis alisema mara uundaji huo utakapoanza baada ya taratibu zote kukamilika, kiwanda kinatarajiwa kuwa Morogoro na kitakuwa kikiunganisha matrekta 1,000 kwa mwaka na kupunguza pengo la mahitaji ya nyenzo hizo.

“Kwa sasa kuna mahitaji ya matrekta 5,000 kwa mwaka, lakini yanayokuja nchini ni 800 tu. Uunganishaji utakapoanza tutaunganisha matrekta 1,000 na kufikia 1,800 na kupunguza kwa kiasi pengo hilo.

“Matrekta hayo yatakuwa na nguvu tofauti kulingana na uwezo wa mkulima kiuchumi. Tutaunganisha matrekta ya kuanzia nguvufarasi 20 hadi 110. Na zitakuwa zikiuzwa kwa bei ndogo kulingana na ukubwa wa nguvu ya trekta,” alisema Vasileiadis.

Rais wa International Tractors Ltd, Gaurav Saxena alisema  kampuni hiyo imeingia ubia na QGL kwani wamekuwa wakifanya nao biashara kwa muda mrefu na kuunga mkono juhudi za kuendeleza uchumi wa viwanda.

“Tanzania ni nchi ambayo uchumi wake unategemea kilimo, lakini wananchi wake wengi wamekuwa wakitegemea kilimo cha jembe la mkono. Sasa ubia wetu na Quality Group utamsaidia mkulima moja kwa moja, kwani tutakuwa tukiunganisha matrekta ya bei nafuu kulingana na mahitaji ya mkulima.

“Pia, utasaidia kuchochea juhudi za nchi kuelekea katika uchumi wa kati na viwanda, kama ambavyo Rais John Magufuli anavyotaka. Tumefurahi zaidi kwani tutawasaidia wakulima wa madaraja yote kwa kuwapa bidhaa bora zenye ufanisi mkubwa,” alisema Saxena.

Meneja Masoko wa QGL, Timothy Shuma alisema kwa sasa kampuni ipo katika mazungumzo na Serikali kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kupata kibali cha kuanzisha kiwanda hicho na kuanza uzalishaji mara moja Morogoro.

“Tupo katika mazungumzo na Serikali kupata kibali cha kujenga kiwanda Morogoro. Kinatarajiwa kugharimu Sh bilioni 50 hadi Sh bilioni 100. Pia, kitazalisha nafasi za ajira zaidi ya 5,000,” alisema

Mtendaji Mkuu Quality Group apata tuzo India

MTENDAJI Mkuu wa Kampuni ya Qual­ity Group, Arif Sheikh, ametunukiwa Tuzo ya Kiongozi Mkuu-Fahari ya Taifa la India Mwaka 2016.

Sheikh ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Kampuni hiyo kub­wa nchini Tanzania, ametukiwa tuzo hiyo juzi (Septemba 3) mjini Mumbai, India.

Amepata tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya The Asia One Global Indian Leader, baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika kubadili taswira ya sekta ya biashara nchini Tanzania.

Mbali na Sheikh, wengine waliopata tuzo hiyo ni Mwanzishili wa kampuni ya Dangote - Aliko Dangote, Mtend­aji Mkuu wa Kampuni ya Pepsi, Indira Nooyi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Microsoft, Satya Nadela.

Pia, taasisi hiyo ikawatambua na ku­wapa tuzo hiyo, Nita Ambani, Mshindi wa tuzo ya Nobeli, Prof Amartya Sen, Gautam Singhania na Raymond Group.

Kwa nini Sheikh?

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh aliwashukuru wafanyakazi wenzake wa kampuni ya Quality Group Limited, hu­susan mtangulizi wake katika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Yusuf Manji.

“Imekuwa ni heshima kubwa sana kwangu kupata tuzo hii ya kimataifa. In­gawa mimi ndiye niliyepewa tuzo hiyo, ninaitoa kuwa ni fahari ya kampuni ni­nayoiongoza ya Quality Group Limited. Nimefurahi kwamba nimeingia katika orodha ya watu waliowahi kupata tuzo hiyo ambao nimekuwa nikivutiwa nao sana.”

Sheikh alisema ametembea na kufan­ya kazi katika mabara mbalimbali, la­kini kote hajaona kiongozi anayemvutia kama Rais John Magufuli ambaye amea­pa kumuunga mkono katika jitihada zake mbalimbali za kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.

Mashuhuda wasema

Mmoja wa watu waliohudhuria hafla hiyo alitaja kilichomfanya Sheikh afani­kiwe kupata tuzo hiyo kuwa ni uwezo wake wa kuelimisha wengine kutumia taaluma zao kwa ajili ya kujiletea maen­deleo endelevu.

“Amekuwa akifanya shughuli zake kwa kuwashirikisha wafanyakazi wenzake na ukiwauliza wafanyakazi wake watak­wambia kuwa kufanya kazi na Sheikh ni ngumu lakini inakusaidia kuji­funza,” alisema.

Kwa sasa Sheikh anakuza kipawa chake cha kuendesha biashara nchini Tanzania kwa kutekeleza miradi kadhaa ukiwamo mradi wa FastaFasta unaotoa huduma ya usafiri kwa kutumia pikipiki 60,000 na mradi wa kuendeleza Mji Mkongwe ambao utakapoin­gia katika hatua ya tatu, utakuwa moja ya miradi michache inayotoa ajira kwa Watanzania wengi.

Miradi mingine ni Pamoja worlds am­bao ni mradi wa kwanza nchini Tanza­nia unaotoa huduma ya mtandao kwa Lugha ya Kiswahili, biashara mtandao na miradi mingine kadhaa katika sekta zinazoendelea kukua nchini humo iki­wamo sekta ya Elimu, afya, Teknolojia, mauzo ya nje, Magazeti, Kilimo Biashara na uchimbaji wa madini ambazo kwa pamoja zimeleta faida ya Dola Bilioni moja za Marekani

“Kwa pamoja miradi hiyo imeifanya Tanzania kuwa ni nchi yenye fursa nzuri ya kukua kiuchumi, kukuza ajira pamo­ja na kuwa eneo salama la uwekezaji wa kimataifa.”

Source: Jambo Leo